Thursday, 12 August 2010

Aug 13th PlaylistMwanza Mwanza

Ni Hayo Tu

August 13

Fid Q.com
Fid Q - Mwanamalundi

Fid Q Ft Bi Kidude - Juhudi za wasiojiweza

Fid Q Ft Juma Nature - Utaua game

Fid Q Ft Nylon - Wananiita King

Fid Q Ft Qj - Kila siku

Fid Q Ft Mzungu Kichaa - Hey Lord

Fid Q - Temanoleji

Friday, 23 July 2010

Tuheshimu kazi za wenzetu jamani na tuwaite majina sahihi,

Mfano;Garden Boy - Landscape Executive and Animal Nutritionist


House Maid - Domestic Operations Specialist


Typist - Printed Document Handler


Messenger - Regional Business Communications Conveyer


Window Cleaner - Transparent Wall Technician


Temporary Teacher - Associate Tutor


Tea Boy - Refreshments Overseer


Garbage Collector - Public sanitation Technician


Watchman - Area Theft Prevention and Surveillance Officer


Thief - Wealth Redistribution Officer


Driver - Automobile propulsion Specialist


Receptionist - Office Access Control Specialist


Cook - Food Technician and Preparation Officer

Monday, 12 July 2010

MZAZI WA BONGOFLAVA NI BLAZAMENI?
Ukiachilia mbali suala zima la kutupia ulimi pale kati, mixa ming’aro ya ziada kiasi cha kumpiga jeki yule asiyekuwa na mauzo ya kutosha…. Leo namdondosha kwenu ‘HANDSOME’ ambaye yeye binafsi anaamini anashine bila bling bling kwasababu ana Mwili na Sura nzuri na hii ni tangu enzi za analogi hadi digito (SWAGGA)
Anaitwa Dully sykes au Prince Dully sykes a.k.a Blazameni Dully a.k.a Mr Misifa ambaye ametuibukia pande hizi ili kuturimaindi kuhusu Historia ya huu mziki wetu wa Bongo Flava.Huyu Blaza alianza Muziki miaka ya 1994 kipindi cha akina Saleh Jabir, naposema kipindi cha akina Salehe Jabir namaanisha ni enzi zile wasanii wetu wanachukua nyimbo za nje na kuzitafsiri kwa kiswahili.. ni kipindi ambacho kilifuata baada ya kile cha ‘MIE NI MSELA/ NINA KICHWA KAMA PERA/SIWEZI KWENDA JELA/ KWASABABU NA MAHELA…’3 Bila shaka hiki ni kipindi ambacho Ubunifu ulikua umeanza kupewa kipaumbele, naam, hii ni hatua ya 3 baada ya ile ya kuimba nyimbo za nje kama zilivyo, kipindi hicho tulikuwa na wakavaji (hawa ni wale ambao walikua wakiipenda ngoma tu lazima waikariri na waifanye kwenye show zao) so tukawa na vikundi vya Naughty by nature wabongo, Michael Jackson wa bongo, Mc Hammer wa bongo na Vannilla Ice wa Bongo.


Elvis,Michael Jackson,UB 40, ni baadhi ya wale waliomuinspaya(kumvutia kimuziki) huyu Prince wa Bongo Flava.. na alikua akiimba nyimbo zao na kuzicheza kama wao kwenye maafali ya darasa la saba au birthday parties za mitaa yake ya kariakoo, show yake ya kwanza ilipigika ndani ya shule ya Shaaban Robert mnamo mwaka 1996 na huko aliwaambia INFORMER ya SNOW,na Dj alikua P FUNK kutoka shule ya IST (International school of Tanganyika
Dully alipenda kuwa Mwanamuziki mwenye nyimbo zake mwenyewe na sio zile za kuiga,na katika kulikwepa hilo alijitengenezea utaratibu wa kuandika nyimbo kwa kufuata hisia zake yeye mwenyewe kama yeye,kwahiyo hakuwa na jinsi zaidi ya kuibuka maeneo ya studio za Don Bosco mnamo mwaka 1998.


Hata hivyo juhudi zake za kurekodi nyimbo Don Bosco ziligonga Mwamba baada ya kukuta foleni kubwa pale studio na zile nenda rudi za Maproducer wetu.. ‘waliniambia niwalipe Elfu Tano ili nirekodi..na hiyo ndo ilikua bei kamili ya studio, nikawapa na pia kama haitoshi nikanunua hadi Chrome.. tatizo studio ilikua bize halafu mie nilikua na mizuka ya kutosha so sikutaka kuwapa pointi, inshoti niliwapotezea lakini hadi leo ile loss ya ELfu Kumi inaniuma.. © DullyJudgement day(ilirekodiwa Marimba records chini ya Mpishi Mr Chaz) ndo title ya Ngoma yake ya kwanza,kwa bahati mbaya haikufanya vizuri kabisa, hakuna aliyeikubali au kuielewa.. lakini siku zote mwanzo huwa mgumu au vipi? Well,hakuna asiyejua ya kwamba Hustla huwa hachoki kwasababu Nia ya mtu huwa imo ndani ya dhamira yake, so ni yeye wakuitengua au kuitilia mkazo.Dully aliamua kujifanyia research yeye mwenyewe ili akijue kile kilichosababisha Tonge lake lisifike Mdomoni na kabla Udhaifu wake haujamulemea,alibahatika kukutana na Dj Stevie B au ‘SKILLZ’(kitambo hicho alikua anaswagua pale Sugar ray) desemba ya mwaka 99 na ushauri pekee aliopewa ni ‘UNAIMBA VIZURI TATIZO WABONGO WENGI HAWAJUI KIINGEREZA, NADHANI UTAFIKA HUKO UNAKOTAKA KWENDA KAMA UTATUMIA KISWAHILI KWENYE TUNGO ZAKO MDOGO WANGU’
Unajua ukweli huwa unahitaji maneno machache tu, nadhani ndo maana ikaclick fasta kwenye ubongo wa mwanafleva huyu na kabla ya karne ya 21 kuingia tayari alikua ashakutana na Mika Mwamba na kile kibao cha ‘JULLIETTA’ kilitoka na kumtambulisha vyema kwenye Medani ya Mziki.


Bila shaka ukimuuliza Mwanamuziki yeyote ambaye anatamba hivi sasa au ashawahi kutamba kuhusiana na hizi chati zetu za kibongo atakuambia ‘kuhiti sio vigumu,vigumu ni kupakua hits baada ya hits’
Ujio wa Dully Sykes ulikuwa ni wa kipekee,bora na wa maana kabisa na cha kushangaza zaidi ni pale alipoongeza makakamavu na kuziacha sifa zimjenge badala ya kubweteka na ktk kulithibitisha hilo aliendelea kupakuwa mawe ya nguvu kama 1- stori ya ukweli 2- Nyambizi 3- Mr Misifa (alipewa na P Funk hilo jina) 4-Salome
Mwaka 2002 alizindua album yake ya kwanza pale Diamond Jubilee, na uzinduzi wake uliendeshwa kwa style ya NANI ZAIDI?kati yake na T.i.d (Top in Dar) na mpaka tunarudi mitamboni ukumbi mzima ulikua upande wa Dully na hali hio haikunishangaza hata mimi kwasababu kazi za Dully zilikua sio kama zile za KOBE WA JUU YA MTI,yaani hapa namaanisha sio mpaka apandishwe ndo awe juu,so tayari mshajua nani alionekana kidume siku hiyo au vipi? Naomba tukumbuke ya kwamba style hii ya kuwapambanisha Magwiji hawa ilitumika kama njia ya kuwavutia mashabiki, kuwapa hamasa ili wajitokeze kwa wingi ukumbini na wala sio kama hawa jamaa walikua na Bifu kama ambavyo wengi walifikiri hapo mwanzoni au labda minong’ono ya nani mkali Mitaani.


Dully aliendelea kulitetea Taji hilo la Mkali wa Bongoflava kwa kupakuwa Mawe mengine ambayo yote yalihit au bado yanasumbua kwenye chati kama 1-Handsome 2-ladies free 3-kijakazi 4-hi 5-leah 6-tanita 7-Jackie 8-Eva 9- Rafiki 10-Latoya 11-Nakupenda 12-Ningejua 13-Mariah Mariah 14- Bijoux 15- hunifahamu 16-Loudspeaker 17-asha Mapromise 18-Baby Candy 19-Watasimuliwa 20-Miss Tz UK 21-Dhahabu 22- dully’s Chick 23-Kupenda 24-Malaika 25- Tamika 26-Opalina 27-Monalisa 28-Sikutaki tena 29-Papa 30-Tata 31-Shikide (ambayo inahit hivi sasa)
Uandishi wa nyimbo zake haupo kwa ajili ya kukufanya ufikirie sana ili kuelewa kile alichokiimba na uimbaji wake ni kama anafanya Mzaha hivi au unaweza sema hayuko serious lakini ukimtegea sikio zaidi utagundua nia na madhumuni yake ni kukufanya uburudike kwa kupitia sanaa yake na sanaa ni kitu ambacho hakina mipaka kama alivyosema Shaaban Robert, ni ukweli Dully Sykes anasifika kwa kuimba Nyimbo zenye ujumbe mwepesi na nyingi zikiwa ni za mapenzi au kujisifia yeye ni nani lakini ni nyimbo hizo hizo ndo zimemfanya akubalike na pia ninathubutu kusema ni aina ya Nyimbo ambazo Jamii inazielewa na kuzipandisha chati mapema zaidi kuliko zile za ki-u-wanaharakati.
VITUKO.
(1) Sote tunajua Chura anayapenda Maji lakini sio ya moto vivyo hivyo Dully anapenda sifa lakini isiwe na dharau ndani yake, moja kati ya matukio anayoyakumbuka ni pamoja na lile deni la shilingi mia moja ya kitanzania aliyokopeshwa na Mdau mmoja wa kitaani kwake kwa ahadi ya kuirudisha pindi tu akitoka au kufanikiwa kimziki… ‘unajua hakuna kitu cha bure sikuhizi,right?nakukopesha hii shing mia ya nauli leo, lakini naomba if utafanikiwa kimziki unirudishie shing mia yangu… ©Mdau
(deni hilo lilipwa tena kwa kiasi hicho hicho cha fedha miaka mitatu baadaye na hiyo ilitokana na yeye Dully kuwa bize na show nyingi za mikoani)
(2) Anasifika kwa kulamba lipsi zake na pia anahisi wasanii wengi wa bongo fleva wakiongozwa na Yule star wa mmarekani wakuitwa LL COOL J wanamgeza yeye Dully Sykes kulambalamba lipsi zake.
(3) Yeye ni mtu wa kwanza kuleta masuala ya Camp, (alipokuja na Misifaz Camp baada ya kuchoshwa na zile stunt za ZERO BRAIN) anajivunia kwa hilo na kwa upande mwingine anasikitika kwasababu ni Camp hiyo hiyo ndo iliyozaa na kulea asilimia kubwa ya Madansa na pia ni Misifaz Camp hiyo hiyo iliyosababisha watoto wa dogo watoboe masikio yao na kuyavika hereni au kujipiga tattoo kabla ya kuwauliza au kupewa ruhusa na wazazi wao, na pia ni Camp hiyohiyo iliyosababisha asilimia kubwa ya Madansa waashie shule za msingi au hata kufukuzwa wakiwa darasa la tatu na kuendelea.
(4) Msanii wa kwanza kupata Skendo mbaya Gazetini.
(5) Ana historia ya kuongea non stop toka mwanzo hadi mwisho wa safari, haijalishi umbali na pia ni Msanii ambaye anaiva na kila Msanii.
(6) Msanii pekee mwenye nyimbo nyingi zenye majina ya kike Duniani (kitabu cha Guinnes hakijamstukia tu)

OUTRO.
Dully ni mfano wa kuigwa mbele ya macho ya mbunifu yeyote sababu huwa haogopi kukosea na ambisheni zake ni zakuongoza sio za ukifuata upepo… hafati ispokuwa anafatwa, na pia ana ujasiri wa kuzitetea hisia na hata kuwaprove wrong wale waliokuwa wanapinga style yake ya Muziki na kuwanyamazisha wale wote waliokuwa wanampaka yeye ni Mwanasesere, Muuza sura tu au Mbana pua..
Wanamuita Mzazi wa Bongo Fleva kwasababu ni yeye ndie aliyeanzisha aina hii ya uimbaji ambao huwa una ladha ya kimwambao na zile za Bangra kwa mbaali (na kama una sikio zuri utagundua kuna vionjo vya kicongo vimeongezwa ili kutia Chachandu siku hizi) na amewainspaya WANABONGOFLAVA wengi na karibia wote wanalikubali hilo pasina kutaka mjadala au kuonyeshana uhodari wa maneno.
Dully anafurahia sana kuona WANABONGOFLAVA wapya wanavyofanikiwa kimaisha na pia anazikubali chalenji zao kwa moyo mweupe kabisa lakini anasema YEYE NI MKONGWE,KAMWE HATOKUBALI KUFUNZWA UTAMADUNI NA WATOTO.
Muziki kwake ni zaidi ya kipaji, yeye binafsi anaamini KIPAJI alichonacho ni kama ZAWADI aliyoshushiwa na Allah ili ajipatie rizki, anamaliza kwakusema ‘alijifunza yeye mwenyewe kupiga gitaa, keyboard na drumz,wala hakufundishwa na mtu yeyote’
Okay…. Baaaaaaaaaiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sunday, 20 June 2010

KHUFU ANKH AMUN

Khufu Ankh Amun has been rapping, recording, & performing since he was six years old. He is a native to New Jersey but has traveled and performed from the small town of Monroe, Louisianna to the well known southern city of Atlanta. He has a style and sound that is so unique that is like nothing you have heard before, his style has been influenced from the traditional to the untraditional. In his early stages he was heavily influenced by artist such as Tupac Shakur who opened his eyes to the injustices been done to black people and those who had fought against them, this had a major impact on Khufu as a youth who was on a path headed for destruction. Artist such as Tupac and Afrika Bambaataa opened Khufu’s eyes to see that he could remain the warrior that he was born to be, but that he could use it to build up and not tear down. In recent years Khufu Ankh Amun has been influenced by his own life experiences calling upon his memories as a reckless but good-hearted youth in the streets, to a now mature, healthy, balanced man who is the provider, protector, and warrior to both his family and his people. Khufu Ankh Amun knows first hand the impact that music can have on people even on a scientific level, and that is why he puts his best foot forward and makes sure as he says in one of his songs that, "...the tones in my music, set my people free". Any who have the priviledge and honor of hearing one of the next upcoming greatest rappers of this time will not soon forget his words and the impact of love and positivity will lingere on in their hearts...an artist such as Khufu Ankh Amun is coming along in a time where music, especially hip-hop/rap ask of the artist to promote and glorify a lifestyle of drugs, disrespect to women, negative thinking, and materialism so Khufu Ankh Amun like many great leaders before comes bringing a message that differs from what is being sold to the people today. Khufu represents a new day and time. Khufu Ankh Amun doesn’t attempt to change the entire world, he simply hopes to offer another way, because if you give people only one option, what choice do they have? but you give people options and you let them choose. And for those who want a change for the better and a higher level of music; Khufu Ankh Amun is that choice.

Contact Information

Artist: Khufu Ankh Amun “Khufu”

Hometown: Camden, New Jersey

Musical Influences: Tupac Shakur, Biggie, Nas, 8 Ball, African Drums, Bob Marley

To Book Khufu Ankh Amun For Live Performance: Call Senkher Kebeht, 580-318-2498 begin_of_the_skype_highlighting              580-318-2498      end_of_the_skype_highlighting or email senkherkebehtmusic@yahoo.com (place the word “Booking” in the subject)

Listen his music on

http://www.myspace.com/khufuankhamun


Tuesday, 15 June 2010

African Hip Hop Thesis kutoka Vijana FM blogMimi kama mpenzi mkubwa wa Hip Hop, nimekuwa nikijaribu kuifuatilia kwa karibu tangia '2 Proud' alipokuwa anavuma na nyimbo kama 'Ni mimi, niko kwenye maikrofoni' na 'Madawa ya kulevya'. Safari ya Hip Hop Tanzania ni ndefu kiasi chake -- ila wengi mtakubaliana na mimi kuwa hatuna "kioo" (as in, standard) madhubuti cha kuangalia na kutath'mini mabadiliko yaliyoletwa na huu muziki wetu.

Mara nyingi mambo mengi tunayojadili kuhusu Hip Hop tunakuwa kama tuna speculate tu. Kwahiyo, tunayoongelea kwenye kijiwe hiki ni tofauti na yatakayoongelewa kwenye kijiwe kingine kutokana na sababu kadhaa.


Fid Q nadhani ameliona hilo na ameamua kufanya utafiti kuangalia Hip Hop kutoka Afrika -- utafiti huu wa kitaaluma utachunguza nini hasa kinachotokea kwenye ulingo wa Hip Hop, mabadiliko kwenye jamii yanayoambatana na Hip Hop, (bila kusahau) Hip Hop kama kitambulisho cha Vijana wengi sasa hivi.

Kilichonifurahisha zaidi ni kwamba anajua wapi pa kuanzia (kwasababu mambo ya utafiti yanahitaji maujanja, na kujua wapi pa kuanzia hurahisisha kazi); ataanza kuongea na wasanii ili kujifunza kama wanafikiri wana nafasi yoyote kwenye jamii.

Mimi binafsi nina maswali mengi mno na nitamuuliza Fid Q maswali machache ili aanze kuumiza kichwa:

1. Marekani inajulikana kama ndio chimbuko la Hip Hop, lakini sasa hivi inaonekana kama Hip Hop inaanza 'kurudi' Afrika (Soma makala kuhusu hili suala hapa). Je, kuna sababu za msingi au ni jambo la kawaida tu?

2. Wasanii wanajua maana ya Hip Hop? Wanaitumia ipasavyo?

3. Niliona filamu moja (documentary) inayozungumzia kufanana kwa maneno ya mitaani kutoka Marekani na Afrika Mashariki (ingawa lugha zitumiwazo ni tofauti). Kuna ukweli wowote ule?

4. Vipi kuhusu mambo yanayozungumzwa kwenye nyimbo mbalimbali. Sehemu mtu anapotoka (msanii) ina athari kubwa sana au ndogo kwenye nyimbo anazoimba? Au hutegemea zaidi mambo fulani mtu aliyopitia kwenye maisha yake binafsi? Ni sahihi kulundika wasanii kutoka Mwanza, Arusha au Dar kwenye kundi moja? Au tuangalie hadi vitongoji wanavyotoka?

5. Kuna baadhi ya wasanii kutoka Tanzania ambao wanaheshimika sana nje ya nchi ilihali bado wanatumia lugha ya Kiswahili kwenye nyimbo zao. Hii inakuwaje? Wengine wanatumia maneno kutoka Temeke!

6. Mabadiliko yanayotokea kwenye Hip Hop yanaakisi yanayotokea kwenye jamii? Au jamii huakisi mambo yanaongelewa na wasanii?

Nitaishia hapa kwa leo.

Ila kama una maswali zaidi au una maujanja yatakayoweza kumrahisishia utafiti huu, unaweza ukamtumia Fid Q barua pepe: cheusidawa@gmail.com. Au unaweza ukatembelea blog yake (ina mipini yake karibia yote; cheki upande wa kulia).

Fid Q, Vijana FM inakutakia kila la kheri! Binafsi, nina uhakika kazi yako itawanufaisha wengi.

Makala nyingine kuhusu Fid Q zinapatikana hapa na hapa...
Imeandikwa na SN

Sunday, 13 June 2010

Power to the Planet
Hi,
I am really interested in the positive hip hop I see coming out of Africa-- so I have decided to write my thesis on hip hop, youth identity and social change.
I am hoping that my research can help to add to the many voices that are drawing attention to all the cool stuff going on, and generate more support for these efforts!!

My initial idea is to focus on how hiphop artists view their role in society. I am looking to talk to various artists - to better understand how they became involved in hiphop and what inspires them to create.

If you have any thoughts, advice, suggestion or if would be willing to talk further please let me know!
I am excited to be able to use my dissertation to learn about the positive efforts going on... look forward to hearing from you Guys.
All the best,